Kujifunza jinsi ya kuweka malengo ni muhimu sana kama ilivyo kujua lengo lenyewe, ukiweza kujifunza jinsi ya kuweka malengo utakuwa umepiga hatua kubwa sana kwasababu utajua unataka nini na utakipataje, watu wengi wanashindwa kufanikiwa aidha kwasababu hawajui kuweka malengo au wanaweka malengo madog
Huu ni muongozo utakao kusaidia kuweka malengo halisiWeka malengo makubwa: Jaribu kupanua mawazo yako kufikiria vitu vikubwa ambavyo kwa kawaida unaona kama hauwezi kuvifikia hivi, fanya malengo yako yawe makubwa iwezekanavyo mpaka ukiyatathmini uogope, maana usipopatwa na hali hiyo ujue unachokilenga kipo ndani ya uwezo wako, jaribu kupanga unataka kuwa nani baada ya miaka 5 au 6 na unataka uweunafanya nini baada ya miaka hiyo
Malengo makubwa yanaweza kutimia itategemea namna unavyofanya kazi kuyatimiza malengo yako
Malengo yako yawe ya uhalisia pia yasiwe yakufikirika sana, hivyo unapopanga malengo jitahidi yawe katikati ya uhalisia na kufikirika, eleza kabisa unataka upate nini na ukipate lini
Katika kupanga malengo kuwa mkweli na muwazi kwako mwenyewe usijiwekee mipaka ukaogopa kuomba msaada, omba msaada pale inapobidi
Katika harakati za kutimiza malengo yako fanya tathmini ya malengo yako kila mara, kitendo hiki kinatakiwa kiwe endelevu usifanye tathmini mwishoniSIFA ZA MALENGO THABITI
Kwanza lazima yawe wazi(specific) yataje unataka nini na kwa wakati gani ili mtu uweze kujua unatafuta nini.
Malengo yawe yanapimika, uwezekupima ni lini unaweza kuyatimiza malengo yako
Malengo yako lazima yaoneshe mpango kazi wako, yani utayafikiaje malengo hayo
Uhalisia, malengo yanatakiwa kuwa makubwa, unatakiwa kulenga mbali sana lakini lazima ujipe changamoto uone uhalisia wa unachokifikiria
Malengo yako yasiwe yakufikirika yawe tangibleHATUA ZA KUWEKA MALENGO THABITI
Weka lengo
Weka mikakati yako itakayokuwezesha kufikia malengo yako
Chagua mkakati bora kuliko yote kati ya hiyo uliyo weka ndio uutumie
Orodhesha wazi mipango ya kukamilisha mkakati wako
No comments:
Post a Comment